Kuna kitu kinaitwa Fantasy world, hii ni dunia ya kusadikika ambayo kiuhalisia hii dunia haipo, dunia hii imetenengenezwa tu kichwani ila kivitendo haipo
Umewahi kuiwaza dunia hii?? Dunia hii ambayo hata klabu ya Simba tuliiweka kwenye dunia hii nami nikiwemo niliamini Simba wapo dunia yao ila ilikuwa ya kusadikika
Tuliwahi kuamini kuondoka kwa Haji Manara basi dunia mpya Simba imeanza kujijengea, dunia ya kuondoka kwenye kelele nyingi na kuhamia kwenye makaratasi zaidi Kama wakubwa wengine Afrika na duniani
Nikaandika makala za kupongeza sana na mapambio kutokana na hatua hiyo ila sasa imenilazimu kula matapishi yangu mwenyewe kwa kile kilichotokea Jana
Kuna misamiati miwili kuna Developing clubs and developed clubs! Kuna klabu inayoendelea na klabu iliyoendelea, lakini Profesa wangu wa Chuo kikuu aliniambia Tanzania hakuna klabu iliyoendelea, ni suala la muda na wasaa tu
Profesa alinikumbusha Kitabu cha SIZITAKI MBICHI HIZI, kisha akamaliza tena na kuniambia hakuna klabu iliyoendelea Tanzania Bali zote zipo kwenye process!
Kwa tafsiri fupi baada ya press ya Jana ni kuwa bado Simba inazimiss kelele za Haji Manara, bado Simba inamiss dunia yake halisi na sio dunia ile ya kusadikika tuliyowatengenezea
Kifupi ni Kama kusema mrithi wa Haji hajapatikana hivyo wamechukua vichwa viwili vya kuungana kisha kuleta flavor kama ya Haji, michambo kama kawaida, ngebe Kama kawaida na kutrend Kama kawaida! Ndio tafsiri sahihi ya nyuma ya pazia
Kwakuwa imechaguliwa style ya INFORMAL (mdomo) basi tunaamini yaliyosemwa Jana na yatakayoendelea kusemwa ndio msimamo wa Simba na Viongozi wao! NIMEKUBALI KULA MATAPISHI YANGU
Kitengo cha Mashabiki na Wanachama kinajifia tunaliona hilo?? Nguvu inawekwa idara ya Habari tu?
Fantasy is the world of imagination, it doesn’t exist