Sukari ya magendo tani 12 zakamatwa Tunduma





Tani 12 za Sukari ya Magendo ambazo zimeingizwa nchini bila kufuata taratibu na sheria zimekamatwa  Mpakani Tunduma kwa ushirikiano mkubwa unafanywa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA Mkoa wa Songwe na Mbeya. 

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ameongoza zoezi la kugawa Sukari hiyo katika taasisi mbalimbali za Mkoa wa Songwe katika shule za bweni, shule za Michezo ,Magereza,Kituo cha watoto yatima,Jeshi la Polisi na Jkt Itaka  ambapo tani 6 zimegawiwa katika taasisi hizo na zingine tani 6 zimepelekwa Mkoani Mbeya.

Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka wafanyabiashara kuachana na biadhara za Magendo kwani kufanya hivyo ni kuendelea kuikosesha serikali mapato. 

Wakati huo huo Mgumba ameipongeza TRA kwa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi na kukusanya kodi bila kutumia nguvu pamoja na kuvuka malengo ya ukusanyaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad