Tasnia ya Bongo Movie Imetawaliwa na Uozo Mkubwa


Tasnia ya Bongo movie imetawaliwa na uozo mkubwa, watu wengi waliojikita katika kiwanda hicho hawana sifa za kufanya kazi hizo.

Kwanza kwenye uandaaji (pre-production) Watu wengi wa bongo movie hawana story za kueleweka, zaidi ya kuungaunga tu story ili kupata cha kuigiza, wengi hawana script ya maana ya kuigizia.

Hawana muda wa kutosha kufanya audition kwaajili ya kupata wahusika wanaoweza kuendana na story yenyewe zaidi ya kupeana uhusika tu kwa kujuana hata kama mtu hana vigezo vya kucheza uhusika Fulani ila anapewa tu kwa kuwa anajuana na Director au ana jina kubwa.

Pili, Wakati wa utengenezaji (production) hawana ratiba maalum ya kushoot wanachokifanya ni kushoot tu kulingana na jinsi muda utakavyowaruhusu kitu ambacho sio professional.

Bajeti walionayo haitoshi kukidhi mahitaji ya location unakuta wanashoot kwa muda mrefu bila kula, kunywa na mahitaji mengineyo.

Tatu, Umaliziaji (post-production) tasnia imejaa maeditor ambao hawana uwezo wa kuleta kitu kipya kwenye editing zaidi ya kurudia yale yale. Wanachojua ni kuunganisha matukio tu ambapo pia wanashindwa kuunganisha matukio na kupata mtiririko unaostahili ili story ieweke kwa watazamaji.

Dondosha Comment yako juu ya uozo uliopo bongo movie, labda watabadilika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad