TBS Yazungumzia Muda wa Matumizi ya Matairi..Mwisho Miaka 8




Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limepiga marufuku matumizi ya matairi ya magari, pikipiki na baiskeli yanayotumika zaidi ya miaka nane tangu yalipotengenezwa.


Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Oktoba 30,2021 jijini Dar es Salaam na ofisa viwango wa shirika hiyo, Arnold Mato wakati akitoa mada kuhusu viwango vinavyotakiwa kwa usalama barabarani katika semina ya waandishi wa habari iliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA).



Amesema tairi la gari, pikipiki na baiskeli haliwezi kudumu kwa zaidi ya miaka nane na hiyo ni kwa sababu matairi huisha muda wake wa matumizi.



"Hivyo tafiti zinaonyesha tairi haliwezi kudumu kwa zaidi ya miaka 10 tangu lilipotengenezwa kiwandani, kwani mpira unaotumika kutengeneza tairi huisha nguvu ikishapita miaka hiyo na matokeo yake upasuka.



"Ndio maana tunasema ili kuepuka kupasuka kwa tairi wakati unaendesha chombo cha moto, epuka kutumia kwa zaidi ya miaka hiyo niliyosema, badilisha kila wakati matairi ya gari lako ili liwe imara zaidi na lisiweze kukusababishia ajali," amesema



Naye mhandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (Tarura), Lutufyo Mwakigonja amesema baadhi ya barabara zinazotakiwa kufanyiwa marekebisho huchelewa kukamilika kutokana na fedha kutotosha.



“Tumekuwa tukipokea simu kutoka kwa wananchi juu ya kurekebisha barabara, tukienda na kukuta marekebisho yanataka fedha kidogo tunafanya lakini yakiwa makubwa hatuwezi kuyafanya kutokana na bajeti,” amesema.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad