Kushoto ni msanii Tommy Flavour, kulia ni Liah
Kutoka Kings Music Records msanii Tommy Flavour amekanusha taarifa za kuiba wimbo wa sitaki tena inayopatikana kwenye Album 'Only One King' ya Alikiba kwa kusema haijawahi kutokea kumdhulumu mtu wimbo wake.
Siku ya Ijumaa msanii wa Mesen Selekta Liah alidai haki zake za kukopiwa verse na melody zinazopatikana kwenye wimbo wake wa doa aliyoitoa miaka miwili iliyopita kutumiwa na Alikiba ambapo muandishi wa hiyo ngoma ni Tommy Flavour.