Tweet ya MO Dewji Kuhusu Kichapo Cha Simba Kwangu Haipo Sawa.. Mo ni Shida Juu ya Shida



Nimezitazama tweet za Mwekezaji wa Simba, MO Dewji kisha nikaona Tweet ya Mzee Magori zote nimeziona kwa uzuri kabisa ila nina shida ya tweet mbili hizi

Tweet ya MO Dewji kwangu haipo sawa, timu imetoka kupoteza ipo katika hali ngumu kisha yeye anakuja kusema kuna watu wawajibishwe, thats not football, kila timu inafahamu kuna matokeo matatu

Nani awajibishwe kama timu bado haina ubavu wa kiuchumi wa kupambana na wakubwa Afrika?? Kama top players ambao ni mhimili wa project wanauzwa nani awajibishwe?

Football ni mchezo wa wazi una namna yake! Kwa mauzo yaliyofanyika na maingizo mapya bado hayajaingia vyema kwenye mfumo niliwahi kusema ni kawaida timu hii kustruggle hapa mwanzoni

Ina maana MO hataki kuheshimu mchakato ambao wao bodi waliuanzisha kwa kuuza?? Nani alilaumiwa wakati Real Madrid walivyomuuza Ronaldo kwenda Juventus? Unamlaumu Kocha au Viongozi? Nani achukuliwe hatua ikiwa wachezaji waliondoka ikiwa yeye ni Mwenyekiti wa bodi?

Wakati TP Mazembe wameingia kwenye falsafa ya PRINCIPLE OF PERCENTAGE RESALE, hawapo vizuri hivi sana hivi sasa kushindana na miamba mingine, umewahi kuona Viongozi wanalalamika?

Simply ni kuwa wanajua wameamua kuuza sana hivyo ni ngumu kutawala Afrika unless project yao ya sasa ikomae! Sasa kama Mazembe wanasubiri ikomae, kwanini MO yeye haamini hilo?

Hizi tweets zinatoa tafsiri halisi ya mpira wetu! Ni sawa na penseli kutuibia kisha unakuja kutusaidia kutafuta! Tatizo halipo kwenye Makocha, tatizo ni huko juu kwenye bodi (Utawala)

Kama mlikubali kuuza basi lazima mkubali timu ijiunde upya taratibu itarejea tena, mnawahi wapi au mlitegemea nini kwa kikosi hiki mapema hii? Kikosi kilindwe na kipewe muda ndio FOOTBALL

Tusihame mada, tubaki kwenye mpira na trusting the process, THATS FOOTBALL
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndugu mwandishi au yeyeto ulieandika hapo juu ukishangaa kuwa wachezaji wawajibike,huna Cha kushangaa coz ikifanya vyema timu hupongezwa vipi wasi wasiwajibishwe hata kwa kusemwa tu ikibidi lazima tukubali mpira una matokeo matatu lakini sio uzembe uwanjani coz Kama stahili zote wanapata pia hamasa IPO vipi wasijitume...tusilee ujinga lazima waambiwe ukweli ikiwezeka wawajibike..we are making step forward we won't toil some fool's to pull us behind.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad