Udsm Kusomesha Wanafunzi 50 Waliofaulu Vizuri Sayansi






CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kinaunga mkono jitihada za serikali katika sayansi kwa kutoa ufadhili kwa wanafunzi 50 wenye ufaulu mzuri katika masomo ya sayansi ambao wamemaliza kidato cha sita.


Makamu Mkuu wa UDSM, Profesa William Anangisye alisema hayo alipokuwa akizungumza na HabariLeo kuhusu mchango wa chuo hicho kwa taifa.



Alisema ufadhili huo utakuwa sawa kwa sawa kwa jinsia zote na haujawahi kuwepo. “Tumetoa ufadhili huo kwa kuwa tunawatia moyo wanafunzi wawekeze kwenye sayansi ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wanafunzi katika masomo hayo,” alisema.



Alisema ufadhili mwingine wanatoa kwa wanafunzi 10 wenye ufaulu wa juu katika shahada za awali ambao nao ni mchango wa chuo hicho katika kusaidia Watanzania.



“Pia tunatoa ufadhili kwa wanafunzi wa kigeni katika shahada za umahiri katika Kiswahili, mpaka sasa walionufaika ni kutoka nchi za Ghana, Rwanda na Uganda,” alisema.



Alisema lengo ni kuunga mkono juhudi za serikali kwa kueneza lugha hiyo nchi za Afrika na duniani kwa ujumla.



Anangisye alisema UDSM inafanya jitihada hizo katika kusaidia serikali kusomesha Watanzania kwani fedha za ndani za chuo hicho ni kwa ajili ya manufaa ya wote

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad