Uhuru awashauri Wakenya 'wakule' pesa za Ruto lakini wafanye uamuzi dhabiti 2022



Rais Uhuru Kenyatta amewashauri wakazi wa eneo la Mlima Kenya kuchukua pesa wanazopewa na naibu Rais William Ruto lakini wawe chonjo wasidanyanganywe na ahadi za uwongo.

Uhuru awashauri Wakenya 'wakule' pesa za wanasiasa lakini wafanye uamuzi dhabiti 2022
Uhuru aliwashauri wakazi hasa wa eneo la Mlima Kenya wachukue pesa kutoka kwa wanasiasa wanaozunguka wakipena kwenye kampeni.Picha:UGC
Akizungumza akiwa Gichugu kaunti ya Kirinya Jumatatu, Oktoba 18, Rais Uhuru aliwahimiza wakazi wawachunguze kwa kina wagombea wote wa urais ambao wanatazamia kumridhi kabla kufanya uamuzi.

Akionekana kumshambulia naibu wake William Ruto, Uhuru aliwashauri wakazi hasa wa eneo la Mlima Kenya wachukue pesa kutoka kwa wanasiasa wanaozunguka wakipena kwenye kampeni lakini watakapoenda debeni wachague viongozi ambao watawahudumia inavyotakikana.

" Lakini wale ambao wanatafuta kura zenu na wanaona wana pesa za kuwapatia, chukua lakini waambie wazingatie na wafikirie kwa undani kabla ya kutoa ahadi ambazo zingine huenda hawatatimiza,"Uhuru alisema.


 
Uhuru ambaye amekuwa akionyesha dalili za kumuidhinisha Raila Odinga kama mrithi wake, alisema kwamba wakazi wa eneo la Mlima Kenya wanapaswa kuchagua viongozi wenyewe sio kulazimishiwa viongozi.

Rais aliwatahadharisha wakazi pia dhidi ya kununuliwa na wanasiasa akidai kwamba mwishowe ni wao wataumia iwapo hawatafanya uamuzi dhabiti.

DP Ruto Kuwafurusha Wanasiasa Wenye Vurugu Katika Chama cha UDA
" Kaeni macho, msije mkanunuliwa na peni mbili, epuka wale wanaozungumza vibaya kuhusu viongozi wenu, msije mkajutia baadaye,"Uhuru aliongezea.


" Msikubali kupotoshwa, wengi wao wanatumia maneno matamu lakini hayazai matunda, mwishowe mwananchi wa kawaida ndiye anaumia na wao wanajinufaisha,"Uhuru aliongezea

Uhuru atarajiwa kustaafu mwaka wa 2022 baada ya kuhudumu kama Rais kwa mihula miwili, wanasiasa kadhaa akiwemo Raila na naibu wake William Ruto wametangaza kukiwania kiti hicho.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad