Ujangili Wa Tembo Wadhibitiwa Kwa Asilimia 90




WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro amesema serikali imefanikiwa kudhibiti ujangili wa tembo kwa asilimia 90. 


Hatua hiyo imewezesha idadi ya wanyama hao kuongezeka kutoka tembo 43,000 miaka kadhaa iliyopita hadi kufikia tembo 60,000 sasa.



Dk Ndumbaro alisema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizochukuliwa na serikali kudhibiti ujangili.



Alipongeza Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania (TAWA), ambao wamekuwa sehemu kubwa ya mafanikio ya udhibiti wa ungajili huo.



Alisema Tanzania imefanikiwa kutokana na hatua zilizochukuliwa ikiwemo kuboresha majeshi, kuongeza vitendea kazi, kubomoa mtandao wa viwanda vya kutengeneza bidhaa zitokanazo na nyara za serikali.



“Nchi imepiga hatua kudhibiti ujangili wa tembo kwa asilimia 90 sasa, haya ni mafanikio makubwa kwetu, ndio maana hivi sasa unasikia hata tembo wameonekana kwenye maeneo kadhaa wakipita au hata kukatiza karibu na makazi ya watu, hiyo ni kwa sababu ujangili umepungua na tunataka tuumalize kabisa,” alisema.



Alisema TAWA pamoja na kuwa ni mamlaka changa isiyo na miaka tangu kuanzishwa kwake, lakini imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kudhibiti ujangili katika maeneo ya mapori tengefu 27 wanayosimamia na maeneo mengine ambayo si hifadhi za taifa.



Ndumbaro alisema kampeni ya kudhibiti ujangili iliyoanza kufanya kazi na serikali mwaka 2016, imeonesha matokeo chanya kwani imefanikiwa kuwadhibiti na kukamata baadhi ya wafanyabiashara wakubwa wa biashara hiyo haramu. Pia imeongeza nguvu ya ulinzi katika hifadhi na maeneo hayo tengefu.



Mwaka 2018 serikali ilianza mpango wa kuwafunga vifaa maalumu tembo katika hifadhi zake ili kufuatilia mienendo yao kama njia mojawapo ya kukabiliana na tishio la ujangili unaosababisha idadi ya wanyama hao kupungua na kutoweka.



Kazi ya kuwafunga vifaa hivyo ilifadhiliwa na wadau mbalimbali likiwemo Shirika la Uhifadhi Mazingira Duniani (WWF) na Friedkin Conservation Fund.



Meneja Mawasiliano wa shirika hilo, Clarence Msafiri alisema walitoa helikopta iliyotumiwa kufuatilia wanyama hao na kuiwezesha serikali kufanikisha kuwafunga tembo hao katika Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.



Awali akizungumzia mikakati yao katika kuimarisha ulinzi dhidi ya ujangili, Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA, Sylvester Mushi alisema wamefanikiwa kuimarisha ulinzi kwa asilimia kubwa dhidi ya ujangili katika maeneo wanayosimamia.



Alisema mafanikio hayo yamechangiwa na juhudi za serikali na vyombo vyao katika kukamata majangili wa tembo na kukata mnyororo wao hivyo biashara hiyo kuharibiwa.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HELLO GET OUT OF FINANCIAL MESS WITH THE HELP OF drbenjaminfinance@gmail.com

    I have been in financial mess for the past months, I’m a single mum with kids to look after. My name is REBECCA MICHAELSON, and am from Ridley Park, Pennsylvania. A couple of weeks ago My friend visited me and along our discussion she told me about DR BENJAMIN OWEN FINANCE of drbenjaminfinance@gmail.com that he can help me out of my financial situation, I never believed cause I have spend so much money on different loan lenders who did nothing other than running away with my money. She advised, I gave it a try because she and some of her colleagues were rescued too by this Godsent lender with loans to revive their dying businesses and paying off bills. so I mailed him and explain all about my financial situation and therefore took me through the loan process which was very brief and easy. After that my loan application worth $278,000.00USD was granted, all i did was to follow the processing and be cooperative and today I am a proud business owner sharing the testimony of God-sent Lender. You can as well reach him through the Company Email drbenjaminfinance@gmail.com

    THANK YOU VERY MUCH

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad