Ujerumani yawarejesha wanawake na watoto waliojiunga na IS




Ujerumani imewarejesha wanawake wanane waliojiunga na kundi linalojiita Dola la Kiislamu IS, sambamba na watoto 23 kutoka Kaskazini mwa Syria. 
Taarifa hiyo imetolewa na wizara ya mambo ya nje, ikiwa ni uhamishaji mkubwa tangu mwaka 2019. Denmark nayo imewapokea wanawake watatu na watoto 14 kama sehemu ya operesheni hiyo iliyotekelezwa kwa kushirikiana na jeshi la Marekani. 

Kabla ya kuletwa hapa Ujerumani, wanawake hao na watoto walikuwa wamewekwa kwenye kambi ya Roj katika eneo la kaskazini mwa Syria linalodhibitiwa na Wakurdi. 

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas amesema watoto hawawajibiki na hali hiyo, ingawa mama zao watalazimika kujibu matendo yao na wamewekwa kizuizini baada ya kuwasili. 

Mara ya mwisho Ujerumani, kwa kushirikiana na Finland iliwarudisha wanawake watano na watoto 18 mnamo mwezi Desemba mwaka 2020

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad