Unaambiwa Hujuma Ndio Chanzo Cha Moto The Cask, Zimamoto Wafunguka




Na Maridhia Ngemela,Mwanza

Hujuma imedaiwa kutumia kwenye ajali ya moto uliotokea kwenye baa ya The cask iliyopo jijini hapa na kutekeleza mali.

Hayo aliyasema leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa.


Kwa mjibu wa kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Mwanza Ambwene Mwakibete amesema uchaguzi uliofanyika umebaini kuwa kuna vitendo vya hujuma vilivyopelekea, sababisha kusababisha mali ya muwekezaji kuteketea kwenye baa hiyo.

Kamanda amesema thamani ya mali zilizohalibika mpaka hivi sasa hazijafahamika lakini kwa kujibu wa kamera zilizofangwa kwenye jengo hilo la biashara la Rock City Mall zinaonyesha kuwa taarifa za moto kama zingetolewa mapema pindi tatizo hilo lilipo anaanza kikosi chake kingeweza kuokoa mali zilizoteketea.



Amesema eneo hilo limefungwa vifaa vya kutolea maji kwa ajili ya kuzima moto pindi ajali itakapotokea.

"Magari ya zimamoto yaliyofika kwenye tukio hilo yakiwa na maji ya kutosha ya kuzima moto kwani kama ungekuwa katika hatua za awali tungeweza kuokoa mali zilizokuwemo kwenye baa hii,"amesema Mwakibete.

Amesema asilimia kubwa ya baa hiyo ilikuwa imejengwa kwa mbao kwani mbao ni kichocho cha moto.

Hata hivyo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema pindi inapotokea ajali ya moto ili kuepusha kusambaa kwa moto na kupelekea mali kuhalibu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad