Unaambiwa Series ya Squid Game Ilikataliwa Kwa Miaka 10 Mpaka Netflix Walipokuja Idhamini



Miongoni mwa series zinazopendwa na kufwatiliwa na wengi duniani kwa hivi sasa ni pamoja na series tokea Korea kusini inayoitwa SQUID GAME iliyoandikwa na kuongozwa na HWANG DONG-HYUK

Iliachiwa rasmi September 17 mwaka huu na hadi kufikia tarehe 13 October imevunja rekodi ya kuwa ndiyo series iliyotazamwa zaidi kwenye mtandao wa Netflix ikifikisha zaidi ya watazamaji milioni 111. Lakini pia ikipata postive reactions za mastaa mbalimbali duniani kama Meek Mill na Burna Boy ambao wanaamini ukiacha kuwa ni movie tu,bali inatupa picha ya aina ya watu tulionao kwenye maisha halisi.

Kwa mara ya kwanza ilianza kuandikwa na Dong-Hyuk mwaka 2009 na baada ya hapo akawa anaipeleka kwenye makampuni mbali mbali ili kupata ufadhili lakini akawa anatolewa nje wengi wakiamini maudhui yake hayana soko hivyo ingewatia hasara, hadi mwaka 2019 Netflix walipokubali kuifadhili. Episode zote 9 zimeandikwa na Dong-Hyuk na kuna wakati aliuza hadi laptop yake aliyoitumia kuandikia series hiyo baada ya kuyumba kiuchumi kutokana na kuhangaikia series hiyo kufadhiliwa.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad