ALIYEKUWA mke wa staa wa RnB Bongo, Ben Pol, Anerlisa Muigai amewalalamikia Wabongo juu ya umri wake na tabia zao za kumuita bibi kizee.
“Watanzania (Wabongo) wanapenda kunitusi na kuniita bibi mzee mara kwa mara, lakini naliacha hilo lipite kwa sababu nitapendelea siku moja wasapoti biashara zetu,” amesema Anerlisa ambaye aliachana na Ben Pol mwaka jana.
Anerlisa mwenye umri wa miaka 34 ni mmiliki wa bidhaa mbalimbali ikiwemo kampuni yake binafsi inayoitwa Nero Limited inayojihusisha na utengenezaji wa maji ya kunywa nchini Kenya.
STORI ZAIDI za AINA HII Download Udaku Spesho App HAPA Iwe Kwenye Simu Yako