Wakili wa Utetezi Aweka Pingamizi Kesi ya Sabaya, Wenzake





Wakili wa utetezi, Fridolin Gwemelo katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya na wenzake sita, Fridolin ameweka pingamizi kupokelewa kama kielelezo cheti kilichowasilishwa mahakamani na shahidi wa saba wa jamhuri ambaye ni ofisa wa Tehama wa benki ya CRDB Kanda ya Kaskazini, Jofrey Abimael Nnko.
Cheti hicho kinaonyesha Sabaya na wenzake walivyorekodiwa katika benki ya CRDB tawi la Kwa Mrombo, Januari 22 kati ya saa 10:09 hadi saa 11:05 ambacho kilikabidhiwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).



Wakili Gwemelo ambaye anawatetea mshitakiwa wa tatu na nne katika kesi hiyo, mbele ya hakimu mkazi, Patrisia Kisinda amenieleza mahakama kuwa, cheti hicho hakionyeshi ubora wa vifaa na mfumo uliotumika.

Wakili Gwemelo amesema bila kuingia katika maudhui ya cheti hicho, kwa kutoeleza tu ubora wa vifaa vilivyotumika kurekodi na kuprint nyaraka hiyo basi ni kinyume cha kifungu 18(3) cha Sheria ya Ushahidi wa Kielekroniki ambacho kimetoa matakwa katika kutoa uthibitisho ya nyaraka mahakamani.

Hata hivyo, mawakili wa Jamhuri, Ofmed Mtenga, Felix Kwetukia na Tarsila Gervas walipinga hoja hiyo kwa maelezo kuwa bado haujafika wakati wa kujadili maudhui ya cheti hicho lakini pia bado mahakama haijakipokea kama kielelezo.

"Hoja hii imekuja mapema na ni kinyume cha sheria, lakini pia upande wa utetezi una nafasi ya kumuhoji shahidi juu ya nyaraka hiyo ambayo kimsingi yeye ndiye ameandaa na anaitambua ndio sababu ameomba ipokelewe kama kielelezo,"amesema wakili Mtenga

Hakimu Kisinda ameahirisha kwa muda kesi hiyo ili kutoa maelezo kupokea cheti hicho ama la.

Awali shahidi huyo, aliieleza mahakama kuwa nyaraka hiyo, aliandaa yeye akiwa katika benki hiyo baada ya kuombwa kufanya hivyo na meneja wa tawi la benki hiyo, Mary Kimasi na maofisa wa Takukuru, Ramadhani Juma na Johnson Kisaka.

Watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad