Wamisionari 15 wa Marekani Watekwa Haiti



TAKRIBAN wamisionari 15 wa Marekani pamoja na familia zao wametekwa na kundi la wahalifu nje ya mji mkuu wa Haiti, Port au Prince.

 

Kwa mujibu wa chanzo cha kiusalama kilichozungumza na shirika la habari la Agence France-Presse, watu kati ya 15 hadi 17 ikiwa ni pamoja na watoto walitekwa na kundi lililojihami kwa silaha.

 

Gazeti la Marekani la New York Times, limemnukuu afisa mmoja wa usalama wa Haiti akisema wahalifu hao walisimamisha basi lililokuwa limewabeba wamisionari hao, likielekea uwanja wa ndege.

 

Kwa miezi kadhaa kundi hilo la wahalifu limekuwa likijihusisha wizi na utekaji kwenye maeneo kati ya Port au Prince na kwenye mpaka na Jamhuri ya Dominica.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad