Wanafunzi wachoma bweni la shule kisa mechi ya Man United Vs Liverpool




Wavulana wanne wa shule nchini Kenya wanashikiliwa katika mahabusu ya polisi kwa kulichoma moto bweni la shule yao, baada ya kuripotiwa kunyimwa ruhusu ya kutazama mechi kati ya Liverpool na Manchester United, umeripoti wavuti wa Daily Nation nchini humo.



Lilimnukuu mkuu wa polisi wa eneo akisema kuwa wanafunzi hao walikuwa miongoni mwa wengine 14 wanohojiwa kuhusiana na tukio hilo.

Wanafunzi hao wanne wanaosoma katika shule ya sekondari yaDr Krapf iliyopo katika eneo la pwani ya Kenya la Kilifi watashitakiwa kwa kosa la kuchoma moto kwa makusudi bweni siku ya Jumatano.



Wanafunzi shuleni wanaruhusiwa tu kutazama televisheni Jumamosi, alisema kamanda wa polisi wa Rabai Fredrick Abuga katika mazungumzo na wavuti wa Daily Nation.

Shule yao kwa sasa imefungwa kufuatia tukio hilo.



Liverpool iliiadhibu timu ya Manchester United kwa kuichapa mabao 5-0 katika uwanjawao wa Old Trafford.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad