Wanaume Maskini Wanaogopa Sana Wanawake Matajiri


Mwanaume hutafuta pesa ili kumridhisha Mke wake na familia ila Mwanamke hutafuta pesa Kama kujikomboa ili ajitenge na mwanaume.

Je unajua sababu za mwanamke kutaka kujitenga? Anajitenga Ili awe na maamuzi ya kujitawala (independent) kwasababu katika nchi za kiafrika, mila zetu zinatufunza kwamba mwanamke lazima awe chini ya mwanaume, lakini utandawazi na harakati za wanawake za kudai haki zao ndio zimefanya wanawake waanze kujitafutia pesa ili waweze kujikimu Kivyao na wasiendeshwe hovyo katika mahusiano kama ilivyokuwa zamani. Kiufupi wanataka kuogopwa na wanaume.

Wanawake wamefanikiwa kiukweli, kuna wanaume wengi wanawaogopa wanawake wenye mafanikio hasa ya kiwango kikubwa cha elimu, fedha, umaarufu au hata madaraka katika jamii. Wanaume wanaogopa kutongoza na hata kuishi nao kwenye ndoa wanawake wa aina hii.

Mwanamke akipata kitu anakuwa jeuri sana. Hawezi kukusikiliza tena na atataka awe huru kufanya mambo yake bila kuingiliwa, uwezo wa kifedha na mafanikio kwenye maeneo mengine ya maisha mara nyingi humfanya mwanamke asiwe na utayari wa kuwa chini ya utawala wa mwanaume. Wewe kama mwanaume Huwezi kuishi na mwanamke anayejiona yuko juu yako na ukabaki salama. Hatokuwa tayari kukupa nafasi ya kuwa na sauti kwenye nyumba.


Kiasili anaeolewa ni mwanamke, hivyo Mwanaume ndiye anayestahiki kuwa juu ya mke wake. Hivyo mwanamke mwenye mafanikio hayuko tayari kuwa chini ya mwanaume anaemzidi elimu au mafanikio. Hapo lazima mahusiano yawe na mgongano.
Ndio maana wanawake wengi wenye mafanikio wanaishi wenyewe tu na watoto wao, ndoa huwa zinawashinda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad