Wasanii Hawa Wana Vipaji Vikubwa Nidhamu Mbaya inawarudisha Nyuma


Wasanii hawa wana vipaji vikubwa na wanaweza kufika mbali zaidi, ila nidhamu mbaya inawarudisha nyuma

1.BARAKA DA PRINCE
Huyu alikuwa anakuja vizuri sana katika tasnia ya bongo fleva mpaka kuna kipindi alikuwa anahofiwa na wasanii wakubwa nchini lakini huyu jamaa ana jeuri kupitiliza, alishawahi kuandikiwa nyimbo na goodluck gozbert na akakana hamjui alipoulizwa.

Pia za chini chini zinadai kuwa alidanganywa ajitoe Rock Star atasainiwa WCB, akaanza jeuri kwa viongozi wake mwisho aliishia kufanya collabo tu na Rommy Jones. Mpaka leo yupo anahangaika kurudi katika peak yake ya mwanzoni ila kipaji anacho, jeuri ndio inamrudisha nyuma.

2.RUBY
Kama kuna msanii wa kike alitakiwa awe billionaire kupitia mziki basi ruby alistahili nafasi hiyo kwa kipaji alichobarikiwa na mpaka sasa hakuna msanii wa kike anayemkaribia kwa kuimba, ila jeuri ndo inamfanya asipige hatua. Kuna kipindi alishawahi kukataa kushiriki FIESTA ambayo inaandaliwa na CLOUDS-watu wenye mchango mkubwa kwenye safari yake ya mziki lakini aligoma kwa madai ya pesa kidogo aliyopewa.

Ruby huyu huyu alishawahi kugoma kufanya video ya SU aliyoshirikishwa na Yamoto Band na ndo sababu iliyomfanya mpaka leo asijiunge na WCB, maana wakati wanatafuta msanii wa kike chaguo la kwanza la diamond lilikuwa RUBY ila viongozi walikataa kwa madai ya kwamba hana nidhamu.

3.YOUNG KILLER
kipaji cha RAP MUSIC kilichopewa kisogo na wadau wa mziki kwa jeuri na kiburi alichonacho cha kuwasema na kuwachana baadhi ya wasanii wenzake.

Huyu kijana pia alitakiwa aende WCB kipindi wasafi wapo katika harakati za kumalizana nae akaanza matusi na dharau kwa CLOUDS hatimae wakamfungia vioo akawa karibu na wasafi mwisho wa siku sio CLOUDS wala WCB wote wamemfungia vioo, yupo anapambana peke yake kwenye kiza kinene na amepoteza mwelekeo kwa siku za karibuni anatoa nyimbo bila mpangilio kwa kukosa mtu wa kumsimamia.

4.HANSTONE
Huyu alianza kuharibu kwanza kwa Boss wake Abbah, kisha akatimkia Wasafi, cha kushangaza kabla ya kusainiwa wasafi ameshindwa kuvumilia kukaa bench na Ameamua kuropoka upuuzi ambao Wadau wa muziki wameona Hanstone Kazingua sana kuwasema vibaya wasafi, Kiufupi hana Uvumilivu.

(Nafasi imeisha,😂😂)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad