Wasifu wa Lengai Ole Sabaya



LENGAI Ole Sabaya amezaliwa 26/12/1986 mkoani Arusha. Amesoma Shahada ya Sayansi katika Elimu Chuo Kikuu cha Mtakatifu John Dodoma (St. John University).

Ole Sabaya aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha na pia aliwahi kushika wadhifa wa Udiwani katika kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha Mjini mwaka 2015.

Ole Sabaya aliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro tarehe 28 Julai 2018 ya aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati John Pombe Magufuli.

Sabaya alitenguliwa nafasi hiyo ya ukuu wa Wilaya ya Hai tarehe 13 Mei 2021 na Rais Samia Suluhu Hassan ili kupisha uchunguzi wa makosa yaliyokuwa yakimkabili ikiwemo unyang’anyi wa kutumia silaha.

 
Tarehe 15 Oktoba 2021 Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Arusha imemhukumu Sabaya na wenzake kifungo cha miaka 30 jela.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad