Wastara: Natamani Diamond Awe Mume Wangu





“BABY wangu, hakuna asubuhi isiyokuwa na usiku na ukiona usiku umeingia ujue mchana unakaribia…”Haya ni maneno ya mwanamama wa Bongo Movies, Wastara Juma kwenye ukurasa wake wa Instagram akisindikizia
na picha ya mwamba wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz.

 

Kupitia intavyu aliyofanya hivi karibuni, Wastara amefunguka mazito huku akisisitiza kwamba ni kweli anampenda mno Diamond au Simba na anatamani siku moja amuoe awe mume wake, jambo ambalo limewashtua mastaa wenzake mbalimbali.

 

Wastara aliandika; “Natamani siku moja Diamond anioe, awe mume wangu…”Kabla ya hapo kuna kipindi aliandika ujumbe mwingine na kusindikiza na picha ya Diamond ampao alimwanikia; “Kukata tamaa ni dhambi. Kuna mwengine haoni ulichonacho ila kuna aliyekiona ulichonacho na anakihitaji hivyo ndivyo mambo yalivyo.”


Wastara ambaye alishaolewa mara kadhaa, kufiwa na mumewe, Sajuki kisha kuachika, amekuwa hafichi hisia zake kwa Diamond na kwamba yupo tayari kuolewa naye.

 

Hata hivyo, Diamond hakuwahi kusema chochote juu ya maombi hayo ya Wastara huku baadhi ya watu wakidai kwamba, huwenda ni kweli anampenda na kushindwa kujizuia pamoja na kwamba umri umekwenda na amejaaliwa watoto kadhaa.Mbali na Sajuki, Wastara amepitia katika maisha ya uhusiano na ndoa kwa wanaume kadhaa.

 


Mwaka 2000 alifunga ndoa na mwanaume anayeitwa Ahmed Kushi kutoka Zanzibar na kuzaa naye mtoto mmoja aitwaye Fares.Nyuma ya hapo, Wastara alizaa mtoto mmoja na msanii wa Bongo Fleva, Msafiri Kondo ‘Solo Thang’.
Mwaka 2003, Wastara alifunga ndoa na Sajuki ambaye alifariki dunia mwaka 2013. Walibahatika kuzaa mtoto mmoja aitwaye Farheen.


Mwaka 2015, Wastara alifunga ndoa na Mbunge Sadifa akitokea kwenye uhusiano na mwigizaji mwenzake wa Bongo
Movies, Bond.Kuna madai kwamba, wakati wa ukimya wake, Wastara alikuwa na mwanaume mwingine ambaye naye wametengana.Hata hivyo, kuna madai pia kwamba, kabla ya kuaga dunia, Sajuki alimsihi Wastara kutoolewa tena na ndiyo maana kila akifanya hivyo, huwa uhusiano haudumu.

STORI: IJUMAA WIKIENDA, DAR

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wastara huna lolote zaidi ya tamaa ya pesa,unajua kwa mondi kuna maisha ndiomana unajilengesha kwake ili ufaidike,ushazeeka unataka kumbemenda mondi?!pambana na hali yako.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad