Jenerali wa ngazi ya juu zaidi wa Sudan anasema jeshi lilichukua mamlaka Jumatatu ili kuepusha vita vya wenyewe kwa wenyewe
Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alisema kuwa makundi ya kisiasa yalikuwa yamewachochea raia dhidi ya vikosi vya usalama
Alisema kuwa amekuwa akimtunza Waziri mkuu aliyeondolewa madarakani , Abdalla Hamdok, ndani ya nyumba yake "kwa usalama wake" lakini kwamba atamrejesha nyumbani kwake Jumanne
Maandamano yanaendelea kwa siku ya pili katika mji mkuu, Khartoum, huku barabara nyingi, madaraja na maduka vikiwa vimefungwa.
Mawasiliano ya simu na intaneti yamevurugika kwa kiasi kikubwa. Takriban watu kumi wameripotiwa kuuawa tangu ghasia zilipoanza.
Thanks for reading Waziri mkuu wa Sudan aliyepinduliwa 'anaishi katika nyumba ‘ya kiongozi wa mapinduzi’