WHO yataka watu wenye kinga dhaifu kupewa dozi ya tatu ya chanjo dhidi ya COVID-19





Jopo la wataalamu wa kimataifa wa afya limeshauri kutolewa kwa dozi ya tatu ya chanjo dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona kwa watu ambao tayari mfumo wao wa kinga umedhoofika.
Wataalamu hao wamesema mjini Geneva kwamba dozi hiyo ya tatu itawahakikishia ulinzi zaidi dhidi ya maambukizi sawa na watu wenye kinga imara waliopata dozi mbili za chanjo.

Kulingana na wataalamu hao kutoka shirika la kimataifa la afya, WHO na kundi la washauri huru wa masuala ya chanjo, SAGE, dozi hiyo inatakiwa kutolewa kati ya mwezi mmoja na mitatu baada ya dozi za mwanzo.

Tume ya chanjo nchini Ujerumani, Stiko, pia inahimiza chanjo ya tatu kwa kundi la watu wenye kinga dhaifu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad