Web

Zari Atoboa Siri "Diamond Platnumz Hajawahi Nioa, Nimeolewa Mara Moja tu Msinipe Presha"


Kwa mara ya kwanza, mwanamama Zari The Boss Lady; baby mama wa staa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz, amevunja ukimya;
🗣“Nimeolewa mara moja tu katika maisha yangu!” Katika mahojiano maalum (exclusive) aliyofanya na Mtandao
wa bizz.com akiwa nyumbani kwao nchini Uganda, Zari anasema kuwa, ndoa pekee aliyofunga ilikuwa kati yake na mumewe, Ivan Ssemwanga ambaye alitangulia mbele ya haki siku ile ya Mei 25, 2017.




Hata hivyo, Kibongobongo, Zari alifahamika zaidi baada ya kuwa mpenzi wa Diamond kisha kuzaa naye watoto wawili, Tiffah Dangote na Prince Nillan ambao kwa sasa wanasaidiana kuwalea, kwani waliachana huku Zari akiendelea na maisha yake nchini Afrika Kusini.

Katika mahojiano hayo, Zari anasisitiza kuwa, hawezi kuacha kuishi maisha yake kwa sababu watu watamsema.
🗣“Nimeolewa mara moja tu Wengine wako wamekwama maishani na bahati mbaya, hawana hata mtu anayewaulizia”

🗣“Sitaacha kuishi maisha yangu kwa sababu kuna mtu atazungumza” Anasema mwanamama Zari ambaye
anatajwa kuwa miongoni mwa wanawake wenye utajiri mkubwa ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Zari anasema kuwa, miongoni mwa mambo ambayo hafurahishwi nayo kabisa ni kuhukumiwa Anasema Zari.




Hata hivyo, mambo hayo yote yanakuja siku chache baada ya Zari kusema kwamba amechoka kueleza watu kuhusiana na maisha yake mitandaoni.

Pia hii ni baada ya ule uvumi kuenea kwamba ameolewa kwa mara nyingine.“Kuanzia sasa nitaweka kile ninachojisikia, kama kitakukera ni-unfollow, nimechoka kuwa mtumwa wa kujieleza kwa nini nafanya kitu f’lani?” Anasema Zari ambaye mara kadhaa amekuwa akishambuliwa na baadhi ya Wabongo ambao amekuwa akipambana nao kila kukicha.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad