Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Namungo vs Yanga Leo


Mambo 10 nilioyaona Namungo vs Yanga

1: That was Too Much Aisee😡 Aibu na Tusi kubwa kwa soka letu kuwa na Mwamuzi wa aina ile kwenye Ligi yetu. Inakera na Inarudisha nyuma juhudi za wanaoutakia mema mpira wa Tanzania

2:Penalti ya mchongo! Emmanuel Charles hakuugusa kabisa mwili wa Feisal Salum.. That was Clean Tackle. Refa Abel William anaweza asiwaombe radhi Namungo.. Lakini kwa wakati wake amuombe radhi Mungu wake kwa tukio lile

3: Sina tatizo na Red Card.. Reaction ya Hamis Khalifa haistahili. Nina tatizo na Ile penalti. Wakati Saido anaupiga ule mpira wachezaji walishaingia ndani ya boksi. Ilitakiwa kurudiwa!

4: Tactically, Benchi la Ufundi la Namungo lilifanya Homework yake vyema kucheza na Yanga. Perfect System.. 4-2-3-1 kama walivyokuja Yanga. tofauti ilikuwa katika sehemu mbili

5: Moja, Style of Play ya Namungo ilikuwa ni kucheza mpira kwa kuutupa mbele haraka wakati Yanga ilikuwa ni kucheza kwa kuuchezea mpira! Pitch ya Ilulu iliwapa Tabu Yanga kwenye aina yao

6: Pili ni kujitoa kwa ya wachezaji wa Namungo. Hapa ndipo Tofauti kubwa ya mchezo ilipokuja. Namungo walipress wote.. Waligombea mipira ya 50/50 na kushinda kwa asilimia kubwa! Yanga ni kama walipigwa na butwaa miguuni kipindi cha kwanza

7: Diarra ✊ What A Perfomance.. Mikono yake iliwaweka Yanga salama muda mwingi wa mchezo! Alikuwa bora kwenye Timing na kuhesabu vyema hatua za mastraika kabla hajautoa mwili wake kuufata shambulizi

8: Well Done Nyenye👏 Amepata kadi nyekundu Lakini ubora wake hauwezi kusahaulika. Alikata vyema mawasiliano ya Bangala na Feitoto katikati ya kiwanja

9: Well Done Emmanuel Charles.. Alikaba vyema na kupandisha mashambulizi upande wa kushoto. Ni yeye aliyempa Kichuya nguvu ya kusogea kwenye Half Spaces kuisumbua beki ya Yanga

10: 'Sub' ya Ntibazonkiza ilichelewa kiwanjani. Kwa viwanja vile unahitaji wachezaji bora kwenye mipira ya kutengwa

Nb: Tumuachie Mungu tu.. 😃
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad