Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Simba vs NAMUNGO"




1: WHAT A GAME.. It's Not Over Until Its OVER.. Ile Fighting Spirit ya wachezaji wa Simba🙌 Jasho walilomwaga ni ishara ya kuthamini machozi ya mashabiki wao.. WELL DONE KWAO👏

2: Simba 🦁 wamepata Pointi 3 Muhimu kuelekea mapumziko ya Ligi. Kuna utulivu utakuwepo katika kipindi hiki viongozi wanapoelekea kufanya baadhi ya maamuzi ya msingi kwa Timu msimu huu

3: AGAIN.. Simba wameonyesha shida kwenye mbinu. Kuna nyakati system yao ilionekana kwenye 4-1-4-1.. Kuna nyakati ikahamia 4-1-3-2 .. Na kuna nyakati ikarudi kwenye 4-2-3-1.. It's Complicated! Ili kushinda mechi katika hali hii, unahitaji kitu kimoja uwanjani. Kipi?

4: Quality. Ubora wa wachezaji uamue mchezo. Hapo ndipo ulipokuja mguu wa kulia wa 'Mr SIMBA'.. IBRAHIM AJIB🙌 WHAT A PLAYER. Ubongo wake ulikuwa 'Active' sana! Alizunguka kwenye maeneo muhimu kusaka mpira na kuuweka katika njia yake

5: Well Done kocha wa Namungo, Hemed Morocco! Tactically alifanya 'Home work' yake vizuri kuijua Simba ubora na udhaifu wao. Alianza na system ya 4-5-1 baadae akaswitch kwenye 4-2-4! Hii ilikuwa na Faida gani?

6: Alianza kwa kuubana uwanja. Kwa presha ya Simba ilivyo kwenye mioyo yao, wangetoka dakika 45 bila bao bila shaka wangerudi kipindi cha pili umakini ukiwa umeshuka.. Then Ingiza bunduki zako kuutanua uwanja

7: Makame! Sikuishangaa kadi nyekundu. Muda mrefu alikuwa uwanjani akimshawishi mwamuzi kumpa adhabu hiyo. Kilichonishangaza ni namna alivyokuwa analalamika baada ya kupewa kadi nyekundu.. Shame On Him!

8: Bocco.. Ooops! Kwa uzoefu wake, sikutegemea angemezwa na presha na kupoteza kiwango chake namna ile.. Nafikiri Hitimana alitakiwa kumtoa uwanjani mapema sana.

9: Yule beki wa kushoto wa Namungo, Emmanuel Charles akalale akijivunia Usiku wa leo🙌. Heshima kwa mikono ya Nahimana.. 👏 Aliiweka Namungo mchezoni mpaka dakika ya mwisho!

10: Presha ya mechi ilikuwa kubwa kwa Refa Nassoro Mwinchui. Mechi iliharibika pale alipoanza kuwa na kigugumizi cha maamuzi. Kuna matukio mengi ya hovyo kayameza mpaka alipokuja kupatia kwa Makame

Nb: Mbona mmenuna.. Mlitakaje kwani😀  
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad