1: POINTI 3.. MABAO 3! Mechi 5, Pointi 15 ✊ Kila hadithi ya shabiki wa Yanga Leo ina mwanzo huo! Kwa kocha Nabi, kuna mwanzo wa tofauti! Kwanini?
2: Kuna maswali mengi aliulizwa na kocha wa Ruvu Shooting, Charles Boniface Mkwasa. Maswali magumu, yenye mitego ya kustaajabisha. Ilihitaji kosa la refa Mwandembwa, kuipa nafuu akili ya Nabi.. Kivipi?
3: Ruvu walikuja na 'System' ya 4-3-3 iliyobadilika kwenye 4-5-1 wakikosa mpira. 'Sapraizi' ya kwanza ya Mkwasa ilikuwa ni kuanza na 'False number 9'. Ruvu bila mpira, Kaheza akadrop kati na kuongeza idadi ya viungo katikati
4: Sapraiz ya pili ni 'Role za Shabani Msala na Zuberi Dabi kwenye 'Half spaces' kulia na kushoto, wakitembea pembeni mwa kiungo mkabaji, Ally Mussa Kombo! Hapa Yanga wakakosa Option ya pasi za kushambulia kupitia pembeni
5: Mwandemba ni ishara kuwa kosa moja la Mwamuzi linavyoweza kubadili muelekeo wa mechi ya mpira wa miguu.. HAIKUWA PENALTI. Ishara ya Refa ni kuwa alihukumu lile tukio kwa sababu ya kushika.. Mpira ulimgonga Mayele sio Sonso
6: Mohammed Makaka.. WHAT A PERFOMANCE🙌 Ruvu imepigwa 3 Lakini Ubora wa mikono ya Makaka utasalia kwenye vichwa vya wengi.. Changamoto yake ya kila msimu ni muendelezo wa ubora wake
7: FEITOTO🙌 What A GOAAAL! Ruvu waliimudu akili ya Fei kwenye mfumo Lakini hawakuweza kuondoka na Quality yake mguuni.. Mpira kifuani, shuti la roho mbaya kwa Makaka.. What A Player!
8: Asante Zuberi Dabi.. Asante Shabani Msala.. Jasho lenu lilikuwa na thamani sana uwanjani. Walijitahidi kukimbia sana kiwanjani na kuzingatia nidhamu kubwa ya mchezo licha ya Ruvu kubaki pungufu kiwanjani👏
9: Mukoko.. Yes ni Box To Box mzuri lakini system ya Nabi inahitaji akili ya Aucho kwenye kuihold Timu. Yanga leo ilionekana kuwa na papara licha ya kuwa na Faida ya kuwa wengi kiwanjani
10: WELCOME BACK FARID MUSSA✊ Yacouba anahitaji kupata mechi chache kukaa benchi ili kukumbushwa thamani ya dakika anazochezea kiwanjani
Nb: Ukiwakaba Uwanjani, wanashinda mifukoni kwa Marefa .. 😀