Alikamwe Mambo 10 nilioyaona Simba vs Coastal Union, Coastal walikuwa bora kwa dakika 90 zote kiwanjani



1: BRAVOO COASTAL Union👏 Ni dhambi kubwa ya mpira, kuanza kuikosoa Simba kabla ya kuisifia Coasta Union.. What A Perfomance Mangushi✊ Tactically, Mentally, Coastal walikuwa bora kwa dakika 90 zote kiwanjani

2: Kama kuna kirusi kikubwa kinachoitafuna Simba hivi sasa ni PRESHA! Umakini umepotea kwa wachezaji. Uoga umeshamiri! Wingi wa Shot Off Target ni ishara ya wachezaji kucheza wakiwa na 'Stress' vichwani mwao

3: Melis Medo👏 Mkoba wa yule kocha wa Coastal Union ulishiba mipango mingi ya kunufaika na presha ya Simba.. 'System' ya 4-5-1 kwenye Mid Block iliwapa viungo wa Simba maswali mengi magumu katikati ya kiwanja

4: Kirusi cha Presha kilianza kulitafuna Benchi la Simba. Hitimana alipoteza mamlaka. Utulivu ukapotea. Vikao vilikuwa vingi sana na wakapoteza muda wa kusoma mchezo na kuja na Plan B

5: Ni ngumu kuchagua mchezaji bora kwenye kikosi cha Coastal Union..Lakini yule kiungo Akpan anajua sana mpira. Mtulivu, hana presha.. Asilimia kubwa ya pasi zake ni mbele

6: Kibu Dennis.. A warrior! Kamwaga sana jasho maeneo mengi ya kiwanja! Bad Luck kwake, Presha ya Simba ni kubwa mabegani mwake. Anapania mengi kichwani kabla mpira haujafika

7: Hance Masoud.. Asante Brother!👏 Simba ni kama walichagua upande wa Kushoto wa Coastal kuwa njia yao Lakini Hance alikuwa bora kuipokea changamoto yao kibabe!

8: Body Language ya Bwalya inaonyesha anapitia msongo wa mawazo! Yuko uwanjani kwa ajili ya kushinda mitihani yake sio ya Timu. Nafikiri anahitaji msaada wa kisaikolojia kurudi mchezoni na kuelewa majukumu yake

9: Bocco! Oooh kuna uchovu na presha ndani yake. Achana na papara yake, movement zake kwenye boksi zilipotea. Alikimbia ulipo mpira na sio kukimbia kutengeneza nafasi za mpira kuingia kwenye boksi

10: Tshabalala na Kapombe miili yao imechoka. Mitego ya wapinzani inategwa nyuma yao. Wakipigwa presha, wanapata hofu ya kupanda.. Wakibaki, nguvu ya Simba kushambulia pembeni inapotea

Nb: Bila Penalti, ni GEITA yenye CEO 😀

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad