Aliyehukumiwa Jela, Azawadiwa Bilioni 57




MAHAKAMA ya Jijini la Chikago nchini Marekani, Ijumaa, Oktoba 31, 2021  imemzawadia dola million 25 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 57 za Kitanzania, jamaa mmoja anayefahamika kama Eddie Bolden, baada ya kukutwa hana hatia wakati tayari alishatumikia kifungo cha miaka 22 jela.

 

Eddie Bolden alihukumiwa mwaka 1994 baada ya kupatikana na kesi ya mauaji ya watu wawili na kuachiwa mwaka 2016 hivyo kutimiza miaka 22 jela, Mahakama nchini humo imebaini uzembe uliofanywa na wapelelezi ambao hawakutaka kusikiliza ushahidi uliotolewa na baadhi ya mashuhuda mwaka 1994 , ambao walionesha kuwa Eddie hakuwepo eneo la tukio bali wakati mauaji hayo yanafanyika Eddie alikuwa mgahawani.


Shilingi bilioni 57 alizolipwa, zinatosha kufidia maisha aliyoyakosa uraiani kwa miaka 22?

 Cc; @bakarimahundu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad