Aliyekuwa Mke wa Halaki wa BEN Pol Afunguka "Sijutii Wala Kujilaumu Kuachana na Ben Pol Nina Mengi ya Kuzungumza ila Sitaki Kumdhalilisha"

 


Aliyewahi kuwa mke wa Msanii wa Bongo Fleva, Ben Pol aitwae Anerlisa yupo nchini Tanzania, amewasili Dar es Salaam muda mfupi uliopita na kufunguka mambo kadhaa ikiwemo ndoa yake na mkali huyo wa muziki.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege (JNIA), @anerlisa alisema hataki kuzungumzia ndani kuhusu suala hilo la ndoa kwa kuwa analinda heshima yake na ya familia yake.

“Hutakiwi kuzungumzia ndoa, kwani siyo kama uhusiano wa kawaida, hata kanisani tuilifundisha hivyo, unatakiwa kuiheshimu,” alisema.

Alipoulizwa kama Ben Pol alikosea kuhusu kuzungumzia ndoa yao hadharani, alisema: “Ndiyo alikosea.

“Sitaki kuzungumza mengi kwa kuwa sitaki kudhalilisha nina Mengi Mno, wala sijutii kuachana naye kwa kuwa katika maisha kila kitu ni darasa.” 
.
.
.
#TimesFMDigital #TimesFmNiBaraka #HujasikiaBado #mgusowajamii📻🎧🎤🔥🔥🔥  

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad