YANGA leo watakosa huduma ya kiungo wake fundi Mganda, Khalid Aucho wakati timu hiyo itakapojitupa
uwanjani kuvaana na Namungo FC.
Timu hizo zinatarajiwa kujitupa kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kujaaupinzani mkubwa.
Huo ni mchezo wa pili kiungo huyo mwenye uwezo wa kuchezesha timu na kupiga pasi kuukosa mwingine alioukosa ni ule dhidi ya Ruvu Shooting.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Cedric Kaze alisema kuwa kiungo huyo alitua nchini juzi Alhamisi usiku akitokea nyumbani kwao Uganda.
Kaze alisema kuwa mara baada ya kutua aliomba kubakishwa Dar kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kutokana
na kujisikia vibaya na kuachwa kambini Avic Town, Kigamboni.
“Aucho ana ruhusa ya viongozi kwa ajili ya kuangalia afya yake ambapo baada ya kuwasili nchini afya yake
haikuwa nzuri akaomba kupata muda wa matibabu.
“Hivyo hatakuwa sehemu ya kikosi chetu kitakachocheza dhidi ya Namungo kesho (leo), ataungana na timu baada ya
kurejea Dar,” alisema Kaze
STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam