TAKRIBAN watu milioni mbili ambao hawajachanjwa kikamilifu dhidi ya Covid-19 wamewekwa chini ya zuio la kutotoka nje nchini Austria huku nchi hiyo ikikabiliwa na kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo .
“Hatuchukui hatua hii kirahisi, lakini kwa bahati mbaya ni muhimu,” Kansela Alexander Schallenberg alisema.
Watu ambao hawajachanjwa wataruhusiwa tu kuondoka nyumbani kwa sababu chache, kama vile kufanya kazi au kununua chakula.
Takriban 65% ya wakazi wa Austria wamechanjwa kikamilifu wakati huo huo, kiwango cha maambukizi ya siku saba ni zaidi ya kesi 800 kwa kila watu 100,000, ambayo ni moja ya juu zaidi barani Ulaya.
Kwa ujumla, Ulaya imekuwa tena eneo lililoathiriwa zaidi na janga hili na nchi kadhaa zinaanzisha vizuizi na onyo la kuongezeka kwa visa vya ugonjwa huo.