Babu Tale: Mkubwa Fella Ajengewe Sanamu






BABU Tale; mmoja wa mameneja wa msanii Diamond Platnumz, ameomba kuwa, meneja mwenzake wa msanii huyo ambaye ni mlezi wa vipaji vya muziki, Mkubwa Fella ajengewe sanamu wilayani Temeke jijini Dar.

 

Hii ni kutokana na mchango wake katika tasnia ya muziki Bongo. Mkubwa Fella amehusika pakubwa katika kuwatoa baadhi ya wasanii ambao kwa sasa wanaheshimika Afrika Mashariki. Miongoni mwa wasanii waliopitia mikononi mwa Mkubwa Fella ni bendi iliyovunjika ya Yamoto Band.

 

Kwa mujibu wa Babu Tale, kando na kujengewa sanamu kama ishara ya heshima kwa kazi yake kwenye tasnia ya muziki, Mkubwa Fella anafaa kuwekewa tamasha na wasanii wa iliyokuwa Yamoto Band.

 

Babu Tale anasema kuwa, Mkubwa Fella alihusika pakubwa katika kulea vipaji vya waliokuwa memba wa Yamoto; Enock Bella, Beka Flavour, Aslay na Mbosso.

 

“Mkubwa Fella anastahili kujengewa sanamu ya heshima. Usiku sijalala kabisa, kwani nilizongwa na kumbukumbu ya safari ya muziki na maisha. Mbali ya kuwakumbuka watu wengi, kichwani mwangu ilikuja picha ya darasa lenye watoto wanne wenye masauti yanayogonganisha mashairi yasiyochosha.

 

“Ni kweli nilikuwa nikiliwaza darasa lenye historia kubwa nalo ni Yamoto Band. Ni miaka mingi imepita tangu kundi hili lililowahi kuwa na mvuto mkubwa livunjike. Na leo sijawaza juu ya kwa nini limevunjika? Bali nimewaza na kutafakari uthubutu, malengo, kujitoa na uwekezaji uliofanywa na Mkubwa Fella.

 

“Kwa hakika matamani kuona kundi hili lilowahi kuundwa na Mbosso, Enock Bella, Beka Flavour na Aslay Isihaka wanaandaa tamasha la kutambua, kushukuru na kumpongeza Mkubwa Fella,” anasema Babu Tale ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kusini- Mashariki mkoani Morogoro.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad