Baada ya kuibwaga Yanga CAS, mchezaji wa klabu ya Simba Bernard Morrison @bm3gh ameeleza namna anavyoithamini klabu hiyo iliyomtambulisha katika soka la Tanzania.
"Kuna mwanzo na mwisho, sote tumekuwa tukingojea uamuzi huu (wema au mbaya), hatimaye umefika na umemaliza mashaka yote na mvutano.
"Nataka tu kila mtu ajue jinsi ninavyoithamini Yanga kwa nafasi waliyonipa ya kuwawakilisha na kuvaa jezi yao. Hakuna mtu hapa Tanzania aliyejua wala kujali kuhusu kazi yangu hadi Luc Aymael aliponileta kucheza hapa Tanzania. Asante Luc kwa kuniamini na kunifanya kuwa mkuu. Kuna msemo huko kwetu Ghana kuwa "Daktari mbaya aliyekutunza hadi daktari mzuri alipofika lazima athaminiwe.
"Hata kama alikuwa mbaya, alikuweka hai mpaka yule bora alipofika, nasema rasmi asante kwa Yanga SC na yeyote aliyenifanya nitabasamu au kunipenda nirudi klabuni kwao, bila kusahau mapenzi niliyoonyeshwa na mashabiki wao," Unasomeka ujumbe wa Morrison kupitia ukurasa wake wa instagram.