Chris Brown Adata na Wizikid, Amwagia Sifa Kem Kem Baada ya Kuimba nae Jukwaani


Saa chache baada ya #ChrisBrown kulishambulia vilivyo jukwaa ndani ya ukumbi wa 02 Arena huko London, Uingereza, hii ni baada ya kupandishwa na #WizKid, mkali huyo ametumia ukurasa wake wa instagram kumwaga sifa pamoja na kushukuru heshima ambayo alipewa na WizKid.

Chris Brown amebainisha kuwa anaona ufahari kwa mafanikio ambayo ameyafikia WizKid huku akiweka wazi kuwa wanaurafiki kwa zaidi ya miaka 10.

Hata hivyo, hii sio mara ya kwanza kwa wawili hao kupandishana jukwaani, Chris Brown aliwahi pia kumpandisha Wizkid jukwaani kwenye show ya Tour yake ya Amsterdam mwaka 2016.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad