Mwijaku anadai degree zake mbili hazimruhusu kumjibu Babu Tale , degree mbili hizo zina heshima kubwa maana amezichukua vyuo vikubwa,MZUMBE na UDSM, hivyo akimjibu ni kujidharirisha maana Babu Tale anaweza zidiwa hata na Mtoto wa Mwijaku, Marichui akili ya kufikiria.
Hasa Mwijaku inabidi uache kutumia majina ya Vyuo Ulivyo soma, ni kama unavidharirisha maana havitoi Degree kwa watu ili wakawe machawa mtaani, waropokaji wasio na mipaka. Huna tofauti na akina Lokole na Baba Levo ambao walikimbia umande kitambo hata kabla jua halijachomoza.
Hakuna kitu kibaya licha ya Degree zako zote mbili ila bado jamii ikawa inakuona kituko. Si vibaya kuwa mpambe, ila upambe wenye manufaa kwa muziki wetu
By Sojamedia