TUZO za muziki Afrika za AFRIMA zimetolewa usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria, huku wasanii wa Tanzania Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Ali Kiba wakishindwa kutamba katika tuzo ya msanii bora wa kiume wa Afrika Mashariki.
Tuzo hiyo iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa wasanii hao, imechukuliwa na Eddy Kenzo wa Uganda.
Wasanii wengine wa Tanzania walikuwa wanawania tuzo hizo katika vipengele tofauti ikiwamo cha msanii bora wa kike Afrika Mashariki ni Nandy, Zuchu,Rosa Ree na Spiece Diana ambapo mshindi wa tuzo hiyo ni Nikita Kering kutoka Kenya.
Wengine ni waandaaji wa muziki Kenny na S2kizzy na Kimambo ambao nao hawakufanikiwa kuondoka na chochote, kwani tuzo ya walikuwa katika kipengele Producer bora wa mwaka.