Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2021 limehitimishwa usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria katika Hoteli ya Eko.
Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Eddy Kenzo, Fally Ipupa, Mr Flavour na wengineo.
Tanzania tumetoka kimasomaso kwenye hafla ya tuzo hizo kupitia kwa @djsinyorita ambaye ameshinda katika kipengele cha 'Best African DJ' 2021.
#DjSinyo, ambaye jina lake halisi ni Mwanaisha Said, mbali ya kufanya kazi hiyo katika shughuli mbalimbali ikiwemo kwenye kumbi za burudani, pia ni mwajiriwa wa kituo cha redio Clouds.
Tuzo za Afrima ambazo zilianza kutolewa tangu mwaka 2015, wawakilishi wengine kutoka Tanzania waliokuwa wanawania mwaka huu ni pamoja na Diamond Platnumz, Zuchu, Rayvanny, Darassa, Nandy, Director Kenny, Rosa Ree, Producer Lizer, Alikiba na Harmonize.