Jamaa anasema moja kati ya vitu ambavyo Watanzania wanapaswa kujivunia ni pamoja na muziki wa Singeli kwa sababu sasa hivi ameweza kuupeleka duniani mwenyewe akianzia Uturuki.
Katika mahojiano maalum (exclusive) na Gazeti la IJUMAA, Dullah anafunguka mambo mengi ikiwemo ishu ya kukesha kwa waganga kuwaloga watu mbalimbali
IJUMAA: Mambo vipi Dulla?
DULLA MAKABILA: Salama kabisa uzima upo.
IJUMAA: Hongera tunaona umefikisha muziki wako hadi Uturuki
DULLA MAKABILA: Namshukuru sana Mungu kwa kila hatua ninayopiga kwenye muziki wangu maana bila yeye siwezi kufanya chochote. Kingine ni mashabiki wangu nawapenda sana na pia nashukuru kwa sapoti yao kwangu na wasanii wenzangu
IJUMAA: Naona wasanii wenzako wa Singeli watapata la kuzungumza maana siyo jambo la mchezo, singeli ilikuwa inafanywa kama muziki wa Uswahilini…
DULLA MAKABILA: Mimi ndiye Mfalme wa Singeli, naichukua Singeli, naipeleka duniani na nimeanzia Uturuki.
IJUMAA: Ila nasikia Dulla unaloga sana, je ni kweli?
DULLA MAKABILA: (anacheka) nani amekuambia? Basi huyo aliyekuambia kwamba mimi naloga atakuwa alijaribu kuniloga akanishindwa
IJUMAA: Hivi umeacha siku hizi kwenda kwa waganga wa kienyeji?
DULLA MAKABILA: Naenda tena sana tu!
IJUMAA: Bado hujapunguza tu kwenda huko?
DULLA MAKABILA: Nisiwe muongo kwa kweli, siwezi kupunguza au kuacha.
IJUMAA: Kwa nini sasa usipunguze?
DULLA MAKABILA: Nina sababu gani za kupunguza?
IJUMAA: inasemeka kwamba Dulla umetengwa na Diamond na Wasafi ndiyo maana unahaha kwa mahasimu wake, huna makao, mara EFM, mara Konde Gang, vipi kwani hebu tujuze kilichopo nyuma ya pazia
DULLA MAKABILA: Unajua nini tusimuangalie Majizzo wala Mondi, wale wakikutana ni marafiki, hata mimi kujimaliza kwenye wimbo wangu najuta maana kuna siku hadi niliwahi kumwambia Mondi yaani mimi najipinda kuimba kwenye nyimbo kumbe ninyi ni wana, mnapiga hadi picha ya pamoja
IJUMAA: Alikujibuje yeye Mondi kuhusiana na kupiga picha na Majizzo?
DULLA MAKABILA: Sikumbuki.
IJUMAA: Vipi sasa kuhusiana na wewe na Mondi?
DULLA MAKABILA: Hatuna tatizo