Eric Omondi Kama Marioo





HOJA ya msanii wa Bongo Fleva anayekiwasha na ngoma yake ya Beer Tamu, Marioo, imeungwa mkono na mchekeshaji wa Kenya, Eric Omonid kuhusu hali ilivyo kwenye soko la muziki Tanzania.

Marioo anasema kuwa wasanii wakubwa Tanzania hawawaungi mkono wasanii wengine hasa wale wachanga na hali hiyo inamuumiza mno.

“Halafu kingine kinachoumiza ni hata hawa kaka zetu, yaani hawatakagi kabisa kutu-support vijana wao, unakuta wanaona bora wawape mashavu ma-underground wa Nigeria au South kuliko sisi ambao tunahitaji baraka zao,” anasema Marioo.

Kauli hiyo inaungwa mkono na Omondi akidokeza kuwa wasanii wa nje wanapata hadhi kubwa kuliko wasanii wa Kenya na kwamba kiwanda cha muziki nchini Kenya kiko mahututi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad