Fahamu Miji Mitano Duniani Ambayo Watu wake 'Hawalali Usiku' Mwendo wa Amsha Popo




Kawaida miji au majiji mengi inapofika nyakati za usiku, huwa kimya, kwa sababu watu wengi wanakuwa wamelala, na shughuli nyingi zinakuwa zimesimama. Lakini ipo miji au yapo majiji ambayo, yanakesha, watu wake hawalali, usiku ni kama mchana na mchana ni kama mchana. Yana miundo mbinu na huduma ambazo wakati wote zinafanya majiji hayo kuendesha shughuli zao.

Wasiwasi ni kuwa kama jiji litakuwa macho usiku kucha kunaenda pamoja na kelele, msongamano wa magari na unywaji wa pombe.

Haya ni baadhi ya Majiji ambayo yanakesha usiku kucha kwa mujibu wa orodha hiyo iliyobainishwa katika utafiti uliofanywa miaka ya hivi karibuni na the world's 24-hour Cities ambapo jiji la London limeshika nafasi ya 17 huku mji wa Paris ukiwa nafasi ya 18 na New York nafasi ya 32.

New York City, New York


New York inajulikana kwa jina lisilo rasmi kama Jiji Lisilolala Kamwe, Usafiri wa wa treni ya chini ya ardhi katika jiji hili haufungwi kamwe, migahawa mingi na baa hufunguliwa hadi saa kumi na moja asubuhi na Kivuko cha feri cha Staten kinafanya kazi karibu wakati wote, Ingawa hutopata shida kupata chakula na burudani wakati wowote katika jiji la New York pia ni vizuri kuzingatia kwamba kuna baadhi ya maeneo ya kuepuka kwa gharama yoyote, kama vile Times Square mbapo ni kama nembo ya mji huo lakini pia ni mtego wa watalii.


Buenos Aires, Argentina


Argentina inaweza kuitwa nchi isiyolala na mji mkuu wake Buenos Aires, huwa na msisimko iwe unataka kucheza dansi, kuangalia muziki wa live, kula chakula kitamu au kubarizi kwenye baa na kunywa mvinyo wa Malbec, huwa kuna mengi ya kufanya kwa saa zote za usiku.

Crobar ni "klabu kubwa maarufu ya muziki inayofanya kazi muda wote wa usiku lakini kama unatafuta sehemu nzuri iliyotulia isiyo na kelele unaweza kwenda El Viejo Almacen, sehemu ya maonyesho ya kihistoria ambapo unaweza kunywa na kutazama wachezaji wa tango wakicheza.

Cairo, Egypt


Orodha ya the world's 24-hour cities unalitaja jiji la Cairo nchini Msri umetajwa kuwa unaongoza katika orodha ya majiji yanayokesha saa 24 kwa siku ulimwenguni ukifuatiwa na miji ya Montevideo, Beirut, Buenos Aires na majiji sita ya nchi ya Hispania ambayo ni Malaga, Zaragoza, Madrid, Barcelona, Valencia na Seville.

Maisha ya usiku na kelele kwa saa 24 kwa siku 7 huko Cairo ni kitu cha kawaida katika jiji hilo lenye zaidi ya wakazi milioni 20. Tofauti na nchi nyingine ambapo neno "maisha ya usiku" ni sawa na pombe, huko Cairo, usiku wa manane huchagua zaidi kunywa kahawa ya Kiarabu, kupata vinywaji laini na marafiki, kukaa kwenye migahawa na kufurahia chakula hadi usiku. Iwapo unatamani kuingia kwenye klabu za muziki za usiku kuna Klabu ya Jazz ya Cairo inayopiga muziki wa band wa Jazz na blues.

Tokyo, Japan


Tokyo mara nyingi ni jiji lenye watu wengi , haijalishi ni saa ngapi za usiku au asubuhi. Unaweza ukaanza jioni yako kwenye baa ya kitamaduni ya "tachinomi" na kupata vinywaji mchanganyiko, pia kuna klabu ndogo kwa ajili ya kusikiliza muziki wa band au kuimba karaoke. Chochote unachoamua kufanya, maisha ya usiku ya Tokyo yatakupa uzoefu bora kwa kuzunguka sehemu moja hadi nyingine na kuna mengi sana ya kuona ukikaa sehemu moja usiku kucha.

Beirut, Lebanon


Beirut ndio maana halisi ya furaha isiyo na kikomo, Tembea bila kupangilia sehemu maalumu na ukae mahali popote panapo kuvutia. Beirut Souks, ni sehemu ya maduka makubwa katikati mwa jiji, ni moja ya maeneo ya kufurahia mida ya usiku, ikiwa utahitaji maeneo ya utalii angalia tamasha lolote la ndani la kuhudhuria, daima huwa moja au mawili yanayoendelea Beirut, bila kujali wakati gani wa mwaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad