Ferguson Hausiki ‘ishu’ ya Kocha United





ALIYEKUWA kocha wa Manchester United, Alex Ferguson, hatahusika kwa namna yoyote katika mchakato wa kumsaka atakayekuwa mkuu wa benchi la ufundi la timu hiyo.

Man United iko sokoni kutafuta kocha mpya baada ya kumtimua Ole Gunnar Solskjaer na Ferguson ni mkurugenzi wa soka klabuni hapo.

Katika hatua nyingine, mabosi wa timu hiyo wameendelea kuhususishwa na makocha mbalimbali, akiwamo Mauricio Pochettino anayeiboa PSG.

Wakati Pochettino akitajwa Old Trafford, nafasi yake pale PSG inatarajwa kuchukuliwa na kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad