Harmonize Katupiga na Kitu Kizito Kumbe Briana ni Demu wa DJ Wake


Kuna uwezekano mkubwa kwamba Harmonize alidanganya Umma kuwa Briana ni mpenzi wake mpya. Inadaiwa sio ukweli, Briana ni demu wa mtu mwingine kabisa.

Mwaka 2020, Dj wa Harmonize @djsevenworldwide alimpost Briana na kupachika caption "Will you marry me" lakini haikuwa story kubwa maana Dj Seven hana influence kubwa mitandaoni ila hii inaonesha kabisa kwamba mwenye uhusiano na Briana ni Dj Seven wala sio Harmonize, labda kama imetokea Harmonize amepindua meza kibabe na kumchukua Demu wa Dj wake.

Ingekuwa kama Dj Seven amechukuliwa demu na harmonize basi ungezuka ugomvi, kama ule wa Kenny na Diamond.

Je ukweli ni upi? Inaamana Mwaka 2020 kipindi Dj Seven anampost Briana, tayari Briana alikuwa demu wa harmonize? Inawezekana vipi Demu wa mtu umpost na uandike caption "will you marry me?", Inaingia akilini kweli?

Sasa kama ni demu wa Dj Seven kwanini Harmonize atangaze kuwa Yeye ndio mpenzi wake mpya? Je Briana alidate kwanza na Djseven then akafuatia Harmonize? Hili pia haliwezekani, hakuna demu anayejielewa harafu adate wanaume wawili marafiki.

Au Harmonize alifanya kiki tu ili kuboost album yake iliyobuma mpaka chitoholi?

Inafikirisha sana lakini kwasasa tuachane na suala hilo Time will tell.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad