Hivi ndivyo Dunia inaitazama Tanzania - Balozi Hoyce Temu




Hivi ndivyo Dunia inaitazama Tanzania - Balozi Hoyce Temu
BALOZI na Naibu Mkuu wa Kituo cha Geneva, Hoyce Temu amesema Dunia inaitizama Tanzania kwa sura nyingine na Mashirika ya kimataifa yameonyesha utayari wa kusaidia agenda mbalimbali za maendeleo ikiwemo ile ya 2025 na ila ya 2030.

Akizungumza leo katika mjadala wa kitaifa kuhusu umuhimu wa diplomasia ya uchumi na ushirikiano wa kimataifa katika kuwaletea wananchi maendeleo, Balozi Temu wadau na mashirika ya kimataifa wamefurahi kuona Tanzania inakuwa mbia katika shughuli za maendeleo.

“Dunia na Mashirika makubwa yanaitazama Tanzania kwa sura nyingine na niseme kauli ya Tanzania sio nyepesi katika korido za mashirika haya,” amesema akiwa Uswizi ikiwa ni siku ya pili tangu aripoti katika kituo chake hicho kipya cha kazi.

Agenda ya 2025 inalenga kusukuma maendeleo ya Tanzania na kufikia uchumi wa kati--malengo ambayo pengine yamefikiwa mapema kabla ya kipindi kilicho tarajiwa. Hata hivyo agenda ya 2030 inahusisha malengo endelevu 17 ya maendeleo (sustainable development goals).


 
Itakumbukwa Tanzania iliasisi malengo haya yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa - UN.

“Tumeanza kutekeleza malengo ya SDG. Huu ni mwaka wa sita bado miaka tisa hii tayari tunahitaji kwenda mchakamchaka kufikia malengo,” Balozi Temu amesema na kudai kuwa maamuzi ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kufungua milango ya diplomasia yamesaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa mipango na malengo hayo.

Shirika la Fedha Dunia (IMF) hivi karibu liliidhinisha kiasi cha Sh trilioni 1.3 kwa ajili ya kupambana na athari za UVIKO-19. Hata hivyo Mfuko wa Kimataifa (Global Fund) uliidhinisha zaidi ya Sh trilioni 2 mwezi Agosti kuimarisha mapambano dhidi ya Malaria na Ukimwi.


Kwa mujibu wa Temu fedha hizi zitasaidia juhudi za maendeleo ikiwemo na kukabili athari za UVIKO-19. “Niseme pia ziara ya Rais Samia Scotland itasaidia kutafuta nguvu ya pamoja katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.”

“Tanzania hatuzalishi hewa ukaa kwa kiasi kikubwa lakini tunaathrika zaidi. Vile vile Idadi ya wananchi inaendelea kuongeza lakini sehemu ya dunia imebaki kuwa ileile hivyo kuna haja ya kutafuta namna ya kudhibiti athari za mazingira kwa pamoja,” amesema.

Kwa sasa Tanzania ni mwenyeji wa Mashirika 23 ya kimataifa. Mashirika haya yameanza kuongeza nguvu na kasi kutekeleza mipango inayoaksi malengo ya serikali ya awamu ya sita.

Balozi Temu amebainisha kuwa mchango wa diplomasia ya uchumi kwa taifa si wa kubezwa na kwamba maamuzi ya serikali kufungua balozi ndogo katika mataifa itachochea ukuaji wa kiuchumi. Akitolea mfano ubalozi mdogo wa Congo, Temu alisema punde ndege za shirika la ATCL zitaanza kwenda Congo na kufungua masoko ya bidhaa.


 
Aligusia pia mgogoro kati ya Tanzania na Kenya na kudai kuwa juhudi za kidiplomasia zilizotekelezwa na Rais Samia zimefungua mipaka ya nchi na hivyo kurejesha biashara baina ya pande mbili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad