Idadi ya vifo yaongezeka katika jengo la Nigeria lililoporomoka





Idadi ya watu waliofariki kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa kubwa linaloendelea kujengwa katika mji wa Lagos nchini Nigeria imepanda hadi 36.

Waokoaji wamekuwa wakitafuta manusura tangu jengo hilo lilipoanguka Jumatatu, lakini hakuna aliyepatikana akiwa hai tangu Jumanne.

Katika siku ya nne ya operesheni ya uokoaji, umati wa watu karibu na eneo la mkasa imepungua.

Mashine za kuchimba zinaondoa vifusi, na kuviweka kando.

Wanafamilia wengi wamefadhaishwa na juhudi za uokoaji.

Wanasema kuwa mamlaka zilichelewa sana kushughulikia mkasa huo na haionekani kuwatafuta manusura.

Vituo maalum vya msaada kwa jamaa za waliopotea viliwekwa saa 48 tu baada ya tukio hilo.

Gavana wa jimbo la Lagos anasema shughuli ya uokoaji inaendelea na kwamba jopo huru limeundwa kuchunguza chanzo cha kuanguka jwa jengo hilo.

Itachapisha matokeo yake ndani ya siku 30.

Kuporomoka kwa majengo ni jambo la kawaida nchini Nigeria.

Wataalamu wanasema ni kutokana na ukosefu wa utekelezaji wa kuni za ujenzi, pamoja na matumizi ya vifaa vya bei ya chini na wafanyakazi wasio na ujuzi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad