Idadi ya waliokufa Sierra Leone kwa ajali ya tangi la mafuta yafikia watu 99



Idadi ya waliokufa kwenye mkasa wa mlipuko wa tangi la mafuta mjini Freetown nchini Sierra Leone imepanda na kufikia watu 99 leo huku mamia wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya na baadhi yao wako kwenye hali mahututi. 


Duru kutoka nchini humo zinasema miili ya watu 92 imehifadhiwa kwenye hospitali ya Connaught mjini Freetown huku watu wengine 30 miongoni mwa waliojeruhiwa wakiwa wameungua vibaya na kuna wasiwasi hawatoweza kupona. 



Mkasa huo wa usiku wa kuamkia leo umetokea baada ya lori kuparimia tangi la kuhifadhi mafuta kwenye kitongoji cha Wellington mashariki mwa mji mkuu wa Sierra Leone, Freetown. 



Meya wa mji wa Freetown amesema madhara na hasara kamili ya ajali hiyo bado haijajulikana lakini polisi na maafisa wengine wa serikali wako eneo la tukio kutoa msaada unaohitajika. 



Rais Julius Maada Bio wa Sierra Leone ambayo yuko Scotland kuhudhuria mkutano wa COP26 amesema amefadhaishwa na kisa hicho na kutuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad