Idadi ya waliouwa Sudan yapanda na kufikia watu 40




Idadi ya watu waliouwa nchini Sudan kutokana na maandamano ya kupinga mapinduzi ya mwezi uliopita imepanda na kufikia 40. 


Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa maafisa wa afya baada ya kijana mmoja aliyepigwa risasi kichwani siku chache zilizopita kufariki. Siku ya Jumatano maandamano yaligeuka kuwa ya vurugu zaidi, ambapo watu 16 walipoteza maisha. Polisi wanakana kutumia risasi za moto na kusisitiza kwamba wamekuwa wakitumia nguvu za kawaidia kutawanya maandamano. 



Siku ya Ijumaa, makundi madogo ya waandamanaji yalikusanyika katika vitongoji kadhaa vya Kaskazini mwa Khartoum na kuweka vizuizi barabarani. Chama cha wanataaluma wa Sudan SPA, kimewasihi raia kuendeleza kampeni ya kupinga mapinduzi. 



Kiongozi wa juu wa kijeshi Abdel Fattah al Burhan mnamo Oktoba 25 alitangaza alivunja serikali ya kiraia na kuwakamata viongozi wake.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad