Msemaji wa Ikulu ya Marekani Jen Psaki amesema Rais Joe Biden atawania tena Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024.
Psaki ameyasema wakati Rais Biden mwenye umri wa miaka 79 alipokuwa akihudhuria sikukuu ya kutoa shukrani katika jimbo la North Carolina. Uungwaji mkono wa Biden umeshuka katika miezi ya hivi karibuni na kuibua mjadala miongoni mwa wabunge wa Democrats kuhusu iwapo Rais huyo atawania muhula mwingine wa uongozi.
Aidha maswali yameibuka kuhusu uwezo wa Makamu wa Rais Kamala Harris wa kugombea Urais katika uchaguzi mkuu ujao iwapo Biden ataamua kutowania tena. Kwa mujibu wa kura ya maoni ya hivi karibuni iliyofanywa na gazeti la USA TODAY, imeonyesha asilimia 28 tu ya Wamarekani ndio wanaomuunga mkono Kamala Harris.