Inshirah Musa: Mwanamke jasiri Mmisri aliyetumiwa na Israeli kuipeleleza nchi yake





Vyombo vya habari vya Misri vimeripoti kwamba jasusi wa Israeli amefariki katika mjini Tel Aviv abaada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa akili.

Bi Inshirah Musa, ambaye baadaye alijulikana kama Dina Ben David, alifariki akiwa na umri wa miaka 87, miezi michache baada ya mtoto wake wa kiume Rafi Ben David kufa kutokana na ugonjwa wa saratani.

Inshirah [Dina] ni nani?
Inshirah alikuwa ni mmoja wa majasusi maarufu katika Mashariki ya Kati na Israeli ilimpatia usaidizi muhimu wa kijasusi tangu wakati wa vita vya mwaka 1967, kabla ya kukamatwa na majasusi wa Misri katika mwaka 1974.

Alizaliwa mwaka 1937 katika jimbo la kusini mwa Misri la Minya na aliolewa na Ibrahim Shaheen wakapata watoto watatu pamoja.

Baada ya uvamizi wa Sinai wa Israeli mwaka 1967, Ibrahim Shaheen, ambaye wakati huo hakuwa na ajira, alitafuta kazi katika ofisi ya masuala ya chakula ya Israeli na alikuwa akilipwa dola 70 kwa mwezi.

Kuligana na Al-Ahram, Ibrahim aliwasilisha suala hilo kwa mke wake, Inshirah, na akakubali. Wawili hao baadaye walipewa mafunzo na Shirika la ujasusi la Mossad, Israel, kutuma taarifa kutoka Cairo.

Ibrahim alipata mafunzo ya aina mbali mbali za silaha.
Ibrahim na familia yake walihamia Cairo, na mke wake na watoto wao watatu wa kiume walisaidia kukusanya taarifa za kijasusi na mipango ya kivita kwa ajili ya Israeli , kulingana na Al-Ahram.



Kuuawa kwa kamanda wa jeshi wa wa Misri
Inshirah anaaminiwa kuisaidia Israeli kumuua mkuu wa majesi wa Misri , Jenerali Abdulmunim Riyadh, aliyefariki Machi1969 katika eneo la mfereje wa maji.

Inshirah na mume wake Ibrahim walisafiri kwenda Israeli mara nyingi kupata mafunzi na jinsi ya kutumia vifaa vya upelelezi na walitoa taarifa muhimu kuhusu vita vya mwaka 1973 ambavyo Israeli ilishindwa.

Huduma za ujasisi za Misri, baada ya upelelezi wa muda mrefu kuhusu mtandao wa Inshirah, zilimkamata Ibrahim pamoja na vifaa vyake vya ujasusi katika mwaka 1974 1974. Inshirah alikuwa Italia wakati alipokutana na majasusi wa Israreli- Mossad.

Alirejea Misri mwezi huo huo huo na kukamatwa na maafisa wa ujasusi wa Misri nyumbani kwake.

Mahakama ya Misri iliihukumu familia yake kifo mwezi Novemba 1974, na Ibrahim na Inshirah walipatinana na hatia ya uhaini na kuhukumiwa kifo, huku mwana wao wa kiume wa kwanza akifungwa jela. Watoto wengine wa kiume wawili walipelekwa katika makazi ya kuwatunza watoto.

Ibrahim alinyongwa, huku mke wake Inshirah akinusurika kuuawa kutokana na ombi la Israel. Alifungwa gerezani kwa miaka mitatu kabla ya kupewa msamahana Rais President Anwar Sadat , Januari 1977 "ili awatunze watoto", kulingana na Al-Ahram.

Maisha yake katika Israeli
Baada ya kupewa msamaha, Inshirah na watoto wake wawili wa kiume walihamishiwa Israeli na kujiunga na dini ya Yuda, ndipo alipobadilisha majina na kuitwa "Dina Ben David".

Kanali Hatim Sabir, mtaalamu wa kupambana na ugaidi, aliiambia televisheni ya Misri Machi 2018 kwamba Inshirax aliyaka kurejea katika nchi yake ya Misri, kwasababu alikuwa na maisha magumu nchini Israeli, lakini ombi lake lilikataliwa na serikali ya Cairo.

Taarifa kumuhusu Inshirah imewekwa katika msururu wa filamu zinazoitwa- kuanguka kwa Beersheb - "The Fall in Beersheb-

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad