IKIWA ni muendelezo wa kesi namba 16/2021 ya Uhujumu Uchumi na makosa ya kupanga njama za kupanga kutekeleza matukio ugaidi na kufadhiri ugaidi, inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu hatimaye shahid wa 7 upande wa Jamhuri amewasili mahakamani leo Novemba 5, 2021 kwa ajili ya kutoa ushahidi wake.
Shahidi wa saba aliyejitambulisha kama Mkaguzi wa Jeshi la Polisi, Omary Mahita ambaye anafanya kazi Idara ya Upelelezi, mwenye umri wa miaka 36 akiongozwa na Wakili wa Serikali, Pius Hilla ameieleza mahakama namna alivyohusika katika tukio la ukamataji wa watuhumiwa watatu wanaotuhumiwa katika kesi hiyo.
Akitoa ushahidi wake mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Joachim Tiganga, Inspekta Mahita amesema alipewa maelekezo ya kuunda kikosi maalum ili kukitia nguvuni kikundi cha watu (watuhumiwa ambao ni Mbowe na wenzake, Halfan Bwire, Mohamed Ling’wenya na Adam Kasekwa maarufu kama Adamoo ) ambacho amedai kilikuwa kinataka kufanya vitendo vya kigaidi maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Mbeya.
Ametaja vitendo hivyo vya kihalifu ni kuchoma vituo vya mafuta, kuzuia barabara, kukata miti, kufanya maandamano yasiyo na kikomo pamoja na kumdhuru aliyekuwa mkuu wa wilaya ya hai kwa Kipindi hicho Lengai Ole Sabaya. Mpaka sasa, Inspekta Mahita bado yuko kizimbani anaendelea kutoa ushahidi wake.
Kwa taariza zaid ya kinacheondelea kujiri mahakamani katika kesi ya Freeman Mbowe, Dar es Salaam na ileya Lengai Ole Sabaya kule Arusha, tufuatilie katika tovuti yetu na Instagram page yetu ya GlobalPublishers.