Ishu ya Usajili wa Chama..Yanga Wamuwahi Akiwa Huko Huko Morocco, Wampandia Ndege




IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amependekeza usajili wa wachezaji wawili na uongozi upo katika hatua za mwisho za kuwafuata nyota hao nchini Morocco.
Hiyo ni katika kuelekea usajili wa dirisha dogo unaotarajiwa kufunguliwa Desemba 15, mwaka huu.

Yanga imebakisha nafasi mbili kati ya wachezaji 12 wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuruhusu klabu moja kuwa na wachezaji 12 wa kimataifa.

Mmoja wa mabosi wakubwa wenye ushawishi ndani ya Yanga, ameliambia Spoti Xtra kuwa kocha ametoa mapendekezo ya kusajiliwa winga mmoja mwenye kasi na uwezo wa kutengeneza mabao kutokea pembeni.

Bosi huyo alimtaja mchezaji mwingine ni kiungo mchezeshaji ambaye hapa anatajwa zaidi Clatous Chama aliyewahi kuichezea Simba kabla ya kutua RS Berkane ya nchini Morocco.

Aliongeza kuwa uongozi wa timu hiyo umemkabidhi jukumu hilo Mkurugenzi wa Uwekezaji wa GSM ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said kwa ajili ya kukamilisha usajili wa wachezaji hao wawili.

“Baada ya mchezo dhidi ya Namungo FC, viongozi na wachezaji wapo katika mapumziko mafupi ya siku mbili. Hivyo katika kipindi hiki hakuna kitu chochote kitakachojadiliwa kuhusiana na timu.

“Uongozi umepanga kukutana haraka kesho (leo) baada ya mapumziko hayo kwa ajili ya kuweka mikakati ya usajili pamoja na kocha ambaye yeye ametoa mapendekezo yake.“

Kocha Nabi amependekeza wachezaji wawili wa kigeni kusajiliwa na kati ya hao yupo winga na kiungo mchezeshaji mmoja mwenye uwezo wa kuchezesha timu, hawa wote wanatokea Morocco.

“Kati ya hao wawili huenda akawepo Chama anayetajwa kuja Yanga katika usajili huu wa dirisha dogo,” alisema bosi huyo.

Hivi karibuni, Injinia Hersi alizungumza na Spoti Xtra kuhusiana na usajili ambapo alisema: “Tumepanga kufanya usajili mkubwa utakaotokana na mapendekezo ya kocha wetu Nabi.

“Chini ya bosi wetu Gharib (Salim Mohammed), tunaamini hakuna kitakachoshindikana kwake, kama tumefanikiwa kufanya usajili mkubwa katika usajili mkubwa ninaamini hatashindwa dirisha dogo.”

Tags

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad